Yanga kuwafuata Mtibwa Sugar Kwa ajili ya Mechi ya Ligi Kuu Ya NBC Tanzania
Yanga kuwafuata Mtibwa Sugar asubuhi
Kikosi cha timu ya Young Africans SC kinatarajiwa kusafiri kesho Jumapili asubuhi kuelekea mkoani Morogoro kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Mtibwa Sugar.
Mchezo huo wa 26, unatarajiwa kuchezwa keshokutwa Jumatatu kwenye Uwanja wa Manungu Complex uliopo Turiani mkoani Morogoro kuanzia saa 10:00 jioni.
“Safari ya kesho itaanzia Makao Makuu ya Klabu yetu pLe Jangwani, ambapo wachezaji wote waliocheza mchezo wa mwisho ambao tulishinda goli 1-0 dhidi ya Kagera Sugar watasafiri.
“Kuelekea mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar, matarajio makubwa ni kuendeleza ushindi kwani tuna rekodi nzuri dhidi ya wapinzani wetu hao hasa tunapocheza nyumbani kwao.
“Mara ya mwisho tulipoenda Manungu Complex kucheza dhidi ya Mtibwa Sugar tuliibuka na ushindi wa goli 1-0, huku rekodi bora ikiwa ni katika mechi saba za mwisho tulizokutana dhidi yao tumeshinda zote.
“Mpaka sasa tunaongoza ligi tukiwa na pointi 68 ambapo tunahitaji pointi nne pekee kutetea ubingwa wetu,” imeeleza taarifa ya Yanga.
Check Also:
Leave a Reply